THIS BLOG IS SPONSORED BY KESOM FREIGHT INTERNATIONAL | AND DOLLYWOOD
Monday, November 23, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Rais Kikwete Aelekea Jamaica
Rais Jakaya Kikwete akipanda ndege usiku wa kuamkia leo tayari kuelekea nchini Jamaica kwa ziara rasmi ya serikali ya siku Mbili.Picha na Freddy Maro/Ikulu
 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Rais Karume Anguruma Unguja
MAKAMU wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,Rais Amani Abeid Karume,akipokea maandamano ya wananchi katika uwanja wa Demokrasia,Kibandamaiti, Mkoa wa Mjini Magharibi,Unguja, jana.Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu/Zanzibar
------
Na Stella Nyamenohi,Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Amani Abeid Karume ameeleza kwa undani yaliyojiri katika mkutano kati yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad na kumtaja kiongozi huyo wa CUF kuwa ni jasiri kutokana na uamuzi wake wa kwenda kuwatangazia wafuasi wake kwamba anamtambua kuwa ni Rais.
Rais Karume alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM)kwa lengo la kuelezea mazungumzo hayo ya kisiasa yaliyofikiwa. Mkutano huo uliofanyika Unguja,ulihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi. Alisema Maalim Seif alimtumia salamu za kumuomba wakutane.“Nikamkaribisha nikasema njoo bwana tena tukazungumza sana.Kuna baadhi wakasema sijui nilimpa chai ya maziwa.
Maneno yale siyo ya kweli,”alisema Karume na kufafanua kwamba kila mmoja alikunywa glasi moja ya maji, hali iliyosababisha kelele za kushangilia kutoka kwa mamia ya watu waliojitokeza katika mkutano huo.Kwa mujibu wa Karume,Katibu Mkuu huyo wa CUF alimwambia kwamba chama chake kimeyaona maendeleo na akasema kama wakishirikiana, wataleta maendeleo zaidi. Aliueleza umati huo kuwa Maalim Seif alisema, “sisi CUF tumewakosa, nanyi mmetukosa. Imefika wakati tusameheane.
Tusahau yaliyopita, tugange yajayo. Hayo ndiyo maneno tuliyozungumza,”alisema Rais Karume. Alisema kutokana na kauli ya kiongozi huyo wa CUF,alizingatia ubinadamu kwamba hata kama mtu amekosana na mwingine kwa miaka 100,mmoja akienda na kuomba kusamehewa, lazima anayeambiwa aseme yameisha. Alisema baada ya mazungumzo hayo,Hamad alimwambia Rais Karume amuombee dua wakati akienda kuwaeleza wanachama juu ya tamko la Baraza Kuu la CUF la kumtambua rasmi.
“Akasema niombee dua, nami nikasema nakuombea kila siku,” alisema Karume na kuendelea kushangiliwa. Karume ambaye kila mara hotuba yake ilikatishwa na vigelegele na sauti za kushangilia, alisema, “kwa niaba yenu wote na wapenzi wa CCM, nataka nimpongeze saana, mheshimiwa Seif kwa ujasiri wake. Maana halikuwa jambo rahisi kama hivi kuzungumza na watu wake ambao siku zote walishaelekezwa hivyo.”
Aliendelea kusisitiza,“alikuwa jabali na jasiri. Si jambo jepesi.Kiongozi ye yote wa siasa lazima afike pahala aseme njia hii haifai.” Rais Karume ambaye alisisitiza anawapenda wapinzani na kuwaona kama vile ni askari Polisi, alisema kitendo hicho kilichofanywa na CUF na CCM kisiwani humo, kitaleta mustakabali mpya katika siasa.Alisema upinzani si ugomvi na wala vita.
“Nawapenda sana hawa wapinzani. Ni kama askari Polisi. Kazi moja kubwa ya wapinzani ni kuwachunga walio madarakani wasipoteze njia. Ndo maana napenda wawepo watuongoze ongoze,” alisema na kusisitiza kwamba anaamini kwamba sasa amani ya kudumu imefika Zanzibar. Alisema matokeo ya mazungumzo hayo, ni mafanikio ya vyama vyote na Watanzania kwa ujumla na wala hakuna mshindi katika hilo.
“Huu si uchaguzi. Ushindi unapatikana kwenye uchaguzi. Amani na utulivu ni wa sisi sote,” aliongeza Rais Karume. Wakati huohuo,Rais alisema baada ya mazungumzo hayo, wapo waliosema lipo jambo lingine lililozungumzwa. Bila kutaja jambo hilo,alihoji,“jipi lingine tuzungumze jamani? Hili la amani na utulivu ni dogo?”Ingawa hakuweka wazi,miongoni mwa mambo ambayo baadhi ya watu walikuwa wakihisi kwamba huenda yamezungumzwa ni suala zima la uundwaji wa Serikali ya Mseto(ya pamoja).Karume alisema,“suala la amani tumehangaika nalo miaka mingapi? Wale wanaobeza ebu tuachieni. Kama kuna jambo jingine, milango iko wazi tutazungumza.Kama kuna lingine lenye mustakabali wa nchi, tutazungumza. Kila jambo lina wakati wake, waamuzi wake na mazingira yake.
Wananchi wa Zanzibar msidanganyike waamuzi ni nyie wenyewe.”Alisema Zanzibar wana utaratibu wao waliojiwekea.Alisema wakubwa wanaweza kupanga,lakini hatimaye uamuzi unatakiwa ufanywe na wananchi.“Naamini jambo lolote zuri la mustakabali hamtakataa,lakini msilazimishwe.”
 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Kp Leo!
 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Bendera
Naibu Waziri wa Habari Joel Bendera akiwa na Mkurugenzi wa MAELEZO Clement Mshana na Mkurugenzi wa AICC Bw Kaaya mara baada ya kufungua semina ya Maofisa Habari Mjini A Town Leo hii.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Kanisa Katoliki Lavuna Zaidi Ya Sh 800 Milioni Dar

KANISA katoliki Jimbo kuu la Dar es Salam limekusanya Sh 806.5 milioni za mavuno ya waaumini wake.

Kanisa hilo, lilikusanya mchango huo na kuukabidha juzi kwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo katika misa ya mavuno iliyofanyaki juzi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea mchango huo, kutoka katika Parokia 60 za jimbo hilo, alisema mafanikio yote ya jimbo hilo yametokana na ukarimu wa waumini wake.

"Nilipoteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa jimbo hili miaka 17 iliyopita kulikuwa na Parokia 20, lakini hadi sasa Jimbo lina parokia 60 haya ni mafanikio makubwa ambayo nguvu kubwa imetoka kwenu,"alisema Pengo.

Pengo alitoa shukrani hizo kwa waumini wake wanaokadiriwa kufikia 1.6 milioni huku akitahadharisha waumini hao kutojigamba kutokana namafanikio hayo kwa kuwa majigambo yanaweza kuharibu kazi ya Mungu.

Alisema pamoja na kuwepo kwa mafanikio ya ujenzi wa parokia 60, bado mahitaji ya Parokia nyingine katika jimbo hilo ni makubwa kutokana na wingi wa waumini wa kanisa hilo.

Katika hatu nyingine Askofu Pengo alitumia muda mwingi kuwasihi mapadri wa kanisa hilo, akiwataka kufanya kazi ya kufuata maadili ya Yesu Kristu.

"Ndugu zangu mapadri wenzangu, tuwaomba waumini watuombee ili tusije tukawa kama Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu kwa kumuuza kwa vipande 30 vya fedha,"alisema Pengo.

Pengo aliwataka mapadre kutumia fedha zinazotolewa na waumini kwa malengo yaliyokusudiwa na kwamba matumizi mabaya ya fedha hizo, yanaweza kuwakatisha tamaa waumini hao.

 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Mwakyembe Akataa Kuzungumzia Hoja Za Rostam Aziz

MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe jana aliamua kutozungumzia sakata la Richmond, na hasa hoja za hivi karibuni za mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ya kutaka uchunguzi mpya wa kashfa hiyo kwa kuwa ripoti ya kamati teule ya Bunge ni ya uongo na haikuwa na baadhi ya nyaraka muhimu.

Katika siku za karibuni, Rostam amenukuliwa akitaka uchunguzi mpya wa kashfa hiyo ufanyike, akipendekeza kazi hiyo ifanywe na jopo la majaji na kwamba endapo jopo hilo litamkuta na hatia, atakuwa tayari kujiuzulu nyadhifa zake zote, hoja ambayo imepingwa kwa maelezo kuwa maamuzi ya Bunge hayawezi kuchunguzwa upya na muhimili mwingine wa dola.

Dk Mwakyembe, mmoja wa wabunge wanaojilikana kama makamanda wa vita ya ufisadi, ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo teule ya Bunge ambayo ripoti yake ilisababisha Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu na mawaziri wengine wawili.

Lakini jana, mbunge huyo wa Kyela alikataa kata kata kuzungumzia suala hilo pamoja na hoja za Rostam.

Dk Mwakyembe aliombwa kuzungumzia suala hilo wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Kyela (KDF), uliofanyika Chuo Cha Ufundi (Veta) jijini Dar es Salaam.

"Hapana siwezi kuzungumza lolote leo hapa ni masuala ya KDF tu... nisingependa kuzungumza mambo ambayo sikupanga kuyasema na wala hayahusiani na mkutano huu,"alifafanua na Dk Mwakyembe.

"Nimetoka Mbeya leo na kule kuna ugeni wa Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa, lakini watu wa Kyela wameniambia nije kwa sababu ya umuhimu wa mkutano huu. Kwa hiyo siwezi kuzungumza mada iliyo nje ya mkutano huu, samahani sana."

Mwenyekiti wa KDF, Gray Mwakalukwa alisema katika ufunguzi wa mkutano huo kuwa lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kuchangia juhudi za serikali katika maendeleo hasa katika elimu.

"Tangu kuanza kwa mfuko huu mwaka 2006 hivi sasa Kyela kuna maendeleo makubwa, hasa katika sekta ya elimu... sasa kuna shule nyingi za sekondari tofauti na kipindi cha nyuma," alisema Mwakalukwa ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) na ambaye alikuwa kamishna wa madini.

"KDF imefanya mengi Kyela, ilinunua vitanda 60 kwa ajili wa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Kiwira Coal Mines, lakini pamoja na hayo tumefanya mengi sana ambayo kuyesema yote inahitaji muda wa kutosha."

 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Karume: Waamuzi Serikali Ya Mseto Zanzibar Ni Nyinyi

ATANGAZA AMANI YA KUDUMU IMEREJEA ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume ametangaza rasmi kuzika uhasama wa kisiasa uliokuwepo kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), akisema suala la serikali ya mseto liko mikononi mwa wananchi.

Tamko hilo la Rais Karume limekuja siku chache baada ya katibu mkuu wa CUF, Seif Hamad Rashid kwenda Ikulu ya Zanzibar kuzungumza naye na baadaye kufanya kitendo cha kijasiri cha kuwatangazia wafuasi wake kuwa chama hicho kimeamua kumtambua Karume kuwa rais wa visiwa hivyo.

Bofya Hapa Kwa Habari Zaidi

 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akifungua jengo la wagonjwa wa n je (OPD) la hospitali ya wilaya ya Tandahimba lililojengwa kwa msaada wa mfuko wa rais wa zamani wa Marekani Clinton akiwa katika zaira ya mkoa wa Mtwara.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kitama wilayani Tandahimba akiwa katika ziara ya mkoa wa Mtwara.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Ziarani Mtwara

 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Mafundi
Mafundi wa mamlaka ya maji safi na maji taka DAWASCO wakizibua chemba ya maji taka kwa kutumia mashine maalum ijulikanayo 'Jeting Machine' katika mtaa wa Mkunguni Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Pasta Peter Ash Apaka Albino Losheni
Pasta kutoka nchini Canada Peter Ash ambaye pia ni mlemavu wa ngozi, akimpaka losheni mmoja wa wanafunzi ya shule ya Msingi Mitindo katika wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza. Pasta huyo alizuiliwa kuingia katika eneo la shule kwa muda wa saa mbili kabla ya kuruhusiwa mwisho wa wiki. Picha na Patty Magubira
 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Miss Africa Nancy Sumary, akiwa na Luca, ambaye ni mmiliki wa jarida na mtandao wa Bongo 5.
Abby wa 'Big Brother' katika pozi la snap na Lebo wa Studio 53 ya Afrika Kusini.
Miss Tanzania Nasreen Karim
Super Model..Flavina Matata
TID akiongea na EATV 'Channel 5'
Ms. Seven
Ms. Seven (kati) akiwa na CodeRed crew

CodeRED Launch Party In Dar

MaDJ maarufu Afrika Mashariki CodeRed, walikuwa ndani ya Zanzibar Room, Hotel Kempiski wakizindua rasmi shughuli zao hapa Bongo. CodeRed, ambao wanajulikana pia kama Kenya No 1 R&B & Hip Hop Dj's, sasa wataanza kutoa burudani mara kwa mara nchini Tanzania, angalau mara moja kwa mwezi na wanatarajiwa kuleta changamoto kwa ma DJ wengine wa Bongo.

 
Mwandishi: haki Tarehe: Monday, November 23, 2009 | kiungo mahususi
Rapa wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Busta Rhymes akiima wakati wa kufunga tamasha la fiesta 2009 jijini Dar es Salaam.

Wasanii wa bongo flava wakitumbuiza kwenye tamasha la Fiesta 2009 juzi usiku viwanja vya Posta Kijitonyama.
Enzi hizo, kikundi cha muziki wa bongofleva ambao ni moja ya waasisi wa muziki huo, HBC lililokuwa likiundwa na Prof Jay, Fanani na Big Willy kama uwanaovyo pichani wakikamua katika tamasha la fiesta one love 2009.
Shabiki aliyeonekana kupawa vilivyo na tamasha la Fiesta juzi usiku,hakufahamika kama alikuwa amelewa ama jinsia zake zinamushkeri ama vipi,watu walionekana kumshangaa sana.
Umati wa watu ukilifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii mbalimbali waliokuwa wakipanda stejini kuburudisha.

Kamuzi La Busta Rhymes Katika Picha Ndani Ya Fiesta One Love 2009

 
Friday, November 20, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Kipanya Leo..
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Dr Shein Azindua Mkapa Foundation
The Vice President Dr.Ali Mohamed Shein greeting the former President of Tanzania Benjamin Mkapa,when he arrived to open the annual meeting of the Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation.Photo Vice President Office
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Adhabu Zenu TFF Zinashangaza
-Kikwete
Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshikilia Kombe la Dunia la Mpira wa miguu baada ya kuwasili jana katika uwanja wa taifa Dar es Salaam

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWENYE UZINDUZI WA ZIARA YA KOMBE LA FIFA LA DUNIA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM 19 NOVEMBA, 2009

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Mheshimiwa Joel Bendera (Mb;)
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe.Chiku Garawa;
Waheshimiwa Wabunge;
Wawakilishi wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA;
Viongozi wa Kampuni ya Coca-Cola;
Viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF;
Wageni Waalikwa;Mabibi na Mabwana

Najisikia mwenye furaha kubwa kupata fursa hii ya kujumuika nanyi katika tukio hili la kihistoria kuhusu ziara ya Kombe la FIFA la Dunia hapa Tanzania.Nchi yetu imebahatika, kwa mara nyingine tena, kupata ugeni huu mkubwa wa Kombe la FIFA la Dunia ambayo ndiyo tuzo ya juu inayotolewa kwa nchi bora kuliko zote katika soka duniani.

Hii ni mara ya pili sasa kwa FIFA kutupa heshima hii. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006.Napenda kuwashukuru FIFA na Coca- Cola kwa upendeleo huo kwa nchi yetu.Kabla ya FIFA na Coca-Cola kuanzisha ziara ya Kombe la FIFA la Dunia, wapenda soka wengi duniani walikuwa wanaliona kombe hili kupitia kwenye picha za magazeti na luninga.


Leo hii kupata bahati ya kuliona kombe lenyewe “live” ni jambo la kihistoria litakalodumu katika kumbukumbu yetu kwa miaka mingi. Naipongeza FIFA kwa kuanzisha utaratibu huu wa kuwezesha maelfu ya wapenda soka duniani kuliona kombe hilo kwa karibu na wengine hata kupata nafasi ya kulishika na kupiga nalo picha.


Hii ni fursa ya pekee na ya kujivunia. Kwa Watanzania wenzangu tuichukulie ziara ya Kombe la Dunia nchini mwetu kama ni changamoto kubwa kwetu inayotutaka tufanye vizuri zaidi katika soka ili tulingane nayo heshima hii tuliyopewa.


Hasa ni changamoto kwa viongozi wa soka wa ngazi zote pamoja na wachezaji na wapenzi wa mpira wa miguu nchini. Kuja kwa kombe hili ni deni kwetu na kulilipa kwetu sisi ni kuzinduka, tuendeleze kiwango chetu cha soka nchini ili na sie siku moja tushiriki fainali za kombe hili.


Hili ni jambo linalowezekana. Wapo wenzetu Afrika wameweza, kwa nini sisi tusiweze. Wao ni watu kama sisi, maadamu wameweza na sisi tutaweza. Lakini, ili tuweze hatuna budi kuiga mfano wao hususan waliyofanya na wanayoendelea kufanya kuendeleza mpira wa miguu. Twende tukajifunze kutoka kwao.
Lakini hata kabla ya kwenda huko, yapo mambo ambayo hatuna budi kuyafanya. Naomba nitaje baadhi yake:-


1. Tuimarishe uongozi, utendaji na uendeshaji wa vilabu vya mpira. Mchezaji hufundishwa kucheza mpira katika klabu yake. Hapo ndipo hufundishwa maarifa ya kucheza mpira na vipaji kuendelezwa. Hebu tujiulize hali ya vilabu vyetu vya soka nchini ikoje.
Je vinaongozwa vizuri? Vinaendeshwa vizuri? Jibu tunalijua sote kwamba ni hapana. Lazima suala hili tulitafakari kwa yakini na kulipatia jawabu. Tukishindwa kupata jawabu muafaka na mambo yakaachwa kuendelea yalivyo, mpaka mwisho wa dunia hatutakuwa tumesogea popote.
2. Tupate walimu wenye ujuzi na uzoefu kufundisha timu zetu. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kukuza na kuendeleza vipaji na hivyo kupata wachezaji walio bora.
3. Tuwekeze katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji toka umri mdogo. Vilabu viwe na timu za watoto na vijana. TFF isaidie kuanzishwa kwa shule za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana. Mashuleni wapatikane walimu wa michezo walio wazuri kufundisha.
4. TFF ionekane zaidi ya ilivyo sasa katika mipango ya kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani na hata vilabuni. TFF ikiwa na mipango na ikasimamia na kuwabana wadau kuitekeleza itasaidia. Vinginevyo TFF itabakia kusimama ligi kuu, kutoa adhabu kwa wachezaji, na timu ya taifa.


Hiyo haitoshi.Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi kwa kampuni ya Coca-Cola kwa mchango wake muhimu inaotoa kuendelea mchezo wa soka nchini na hasa soka la vijana. Mashindano ya Kombe la Copa Coca-Cola kwa vijana wa chini ya miaka 17 ni ushahidi tosha wa mchango huo adhimu.


Mashindano hayo yamegusa vijana wengi kote nchini.Naambiwa zaidi ya timu 1500 zilijitokeza kwa mwaka huu na maelfu ya vijana walijitokeza kuonyesha vipaji vyao. Naomba utaratibu huu uendelee kwani utakuwa na manufaa makubwa siku za usoni.
Maombi yangu kwa TFF ni kujipanga vizuri kutambua vijana wenye vipaji vizuri na kupanga mipango ya kuiendeleza.Ujio kwa Kombe la FIFA la Dunia hapa nchini mbali na kuhamasisha vijana wetu pia ni fursa nzuri ya kutangaza nchi yetu pamoja na fursa zake za utalii na uwekezaji.


Watu wengi zaidi wataifahamu nchi yetu vizuri zaidi kupitia ziara hii ya Kombe la Dunia. Hivi sasa tuna uwanja mpya wa kisasa ambao utaonekena vizuri wakati wa ziara hii na pengine kuvutia timu kubwa duniani kuja kufanya mazoezi hapa wakati wa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini 2010.


Changamkieni fursa hii kwa maslahi ya taifa letu ili tunufaike na sisi. Baada ya kusema maneno haya machache, sasa niko tayari kufanya kazi iliyotuleta hapa sote. Nawashukuruni kwa kunisikiliza.

 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Ripoti ya Idadi ya Watu Duniani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Batilda Burian akizinduwa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani Kulia Mwakilishi wa (UNFPA) Nchini Tanzania Dk Juliha Onabanjo katika ofisi za UN Kinondoni Dar es Salaam.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Kwa Mwendo Huu Kipindupindu
Kitakwisha?
Mkazi wa Msasani Bonde la Mpunga Dar es Salaam akiosha vyombo anavyotumia katika mgahawa wake wa kuuzia chakula uliopo karibu na dimbwi kubwa la maji jana jambo ambalo ni hatari kwa afya za watu.Picha na Mroki Mroki
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Nnauye Ahadharisha Wauza
'unga' Kufadhili Vyama
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,Nape Nnauye(Pichani), amesema vitendo watu wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kufadhili vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu,vinasababisha serikali inayoingia madarakani kutekeleza matakwa ya wafadhili hao.

Nape alisema hayo jana jijini Dar es Salaam,alipokuwa akizundua Chama Kuweka na Kukopa cha Upendo Group ambapo alisema serikali inayochaguliwa kwa njia hiyo itakuwa ya wauza madawa ambao maamuzi yao hayawezi kuleta maendeleo kwa wananchi.

“Hao wauza unga wanapopata nafasi ya kukifadhili chama cha siasa kisha chama hicho kikafanikiwa kuingia madarakani kwa nguvu za pesa zao,serikali ya chama hicho haitakuwa na uwezo wa kuwachukulia hatua watu hao na badala yake,itafanya maamuzi kwa muujibu wa wafadhili hao,”alisema Nnauye.

“Tukumbuke waswahili walisema “anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua tuni ya muziki,wafadhili wa aina hiyo wakifanikiwa kukiweka chama madarakani kwa njia fedha zao,wanaweza kuichagulia serikali mambo ya kufanya kwa mgongo wa fedha zao,” alisema.

Kwa muda sasa, kumekuwa na hoja kuwa vyama vya siasa nchini,vinategemea kupata fedha za kampeni kutoka kwa wafadhili wao bila kujali nyanzo vya fedha hizo na athari zake kwa taifa.Hata hivyo Nape ambaye alitoa Sh1.2milioni ili kukiwezesha upendo group kufungua saccos yao alisema vyama vya siasa visivyo kuwa makini na watu hao kuna siku vitajutia.Imeandikwa na Jackson Odoyo.

 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 20, 2009 | kiungo mahususi
Zain Waipa Shavu Fiesta
Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mikononi ya Zain Tunu Kavishe akimkabidhi mtangazaji wa Clouds Fm Ephrahim Kibonde (kwa niaba ya Clouds Media Group),makao makuu ya Zain,kifurushi kama zawadi kwa ajili ya kuwapa watoto yatima na waishio katika mazingira magumu,huo ukiwa katika mchakato mzima wa kauli mbiu ya FIESTA HISANI,mchakato huo umefanyika jana ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo.Kampuni ya Zain ni moja ya wadhamini wa tamasha la fiesta one love linalotarajia kufanyika keshokutwa,jumamosi katika viwanja vya posta,kijitonyama jijini Dar.
 
Wednesday, November 18, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
Ziara Ya Mama Kikwete Singida
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)akiwa amebeba kibuyu mara baada ya kukabidhiwa na wanawake wa kabila la wataturu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika mkoa wa Singida.Mama Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.Picha na Juma Kengele-Ikulu
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
Rais Kikwete:Wazee Hawana
Nafasi 2010..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
---
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwa kama akijaliwa kupata kipindi cha pili cha kuliongoza taifa la Tanzania,atafanya jitihada kubwa kuubadilisha uongozi wa Tanzania kuwa uongozi wa vijana.Rais Kikwete pia amesema kuwa vijana ndiyo Tanzania ya kesho,na kama Tanzania haikuwekeza vya kutosha katika vijana na maendeleo yao,basi itakuwa haiwekezi katika hali yake ya baadaye.
Akizungumza juzi mjini Dar Es Salaam na vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika wanaoshiriki katika Mpango wa Kulea Uongozi wa Afrika wa African Leadership Initiative, Rais Kikwete amesema kuwa anauthamini Mpango huo.


Amewaambia vijana hao ambao wanashiriki katika Mpango huo unaodhaminiwa na Askofu Mkuu(mstaafu)wa Kanisa la Anglikan Desmond Tutu wa Afrika Kusini kuwa kwa kadri miaka inavyokwenda ni lazima rika la wazee lipishe lile la vijana.Rais amewaambia vijana hao kwenye mkutano wao katika Hoteli ya Southern Sun mjini Dar Es Salaam:“Kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, kama nitajaliwa na nikapata bahati ya kuchaguliwa tena,nitahakikisha kuwa naubadilisha uongozi wa Tanzania kwa kuufanya uongozi wa vijana zaidi.


”Ameongeza:“Wale viongozi wa rika langu lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi,na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.”Amesisitiza:“Vijana ndiyo matumaini ya nchi hii katika miaka inayokuja,na kama hatukuwekeza katika vijana wetu,basi ni dhahiri kuwa hatuwekezi ipasavyo katika miaka ijayo ya taifa letu.


”Akijibu maswali ya vijana hao kutoka nchi mbali mbali za Afrika zikiwamo Tanzania,Nigeria, Kenya,Afrika Kusini na Uganda,Rais Kikwete amewaeleza vijana hao jinsi gani alivyojikuta anaingia katika siasa.Akijibu swali kuhusu maendeleo ya karibuni katika siasa za Zanzibar,Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba vyama vya siasa katika Zanzibar vimeamua kuachana na siasa na mazoezi ya zamani na kuanza ukurasa mpya.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
Mheshimiwa Anne Kilango alivyolia
na Wapiga kura Wake Goha
Mbunge wa Same Mashariki,Anne Kilango Malecela akilia kwa uchungu juzi baada ya kufika kijiji cha Goha kulipo tokea maporomoko na kuuwa watu 24 Wilayani Same.
Mheshimiwa Anne Kilango akitembezwa katika eneo la maafa kijiji cha Goha Kitongoji cha Manka juzi.Picha zote kwa Msaada wa Mroki Mroki
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
Rais Kikwete Anguruma
Rome,Italy..
Rais Jakaya Kikwete akinguruma kwenye mkutano wa wakuu wa nchini
kuhusu Usalama wa Chakula nchini Rome
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mh.Ban Ki-Moon jijini Rome leo wanakohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kwa usalama wa chakula
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa FAO Mh. Jacques Diouf na baadaye kufanya maongezi ofisini kwake jijini Rome, Italy
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na rais wa Burundi Mh.Pierre Nkurunzinza ambaye naye anahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu usalama wa chakula duniani jijini Rome,Italy.Picha na Freddy Maro/Ikulu
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
MISA YA KUMBUKUMBU YA
MAREHEMU TOBI aka JIBABA
(MILTON-KEYNES)
----
Milton Keynes TZ Society invites you for a prayer to commemorate our beloved Brother,Family & Friend TOBY aka JIBABA ,Its 3yrs Since His tragic Death,Ceremony will be held on Sat 21st Nov@ Jesus Celeb Centre,Lloyds Court,Central Milton Keynes,MK9 3AT(Formerly Known as Flames) from 2pm-6pm...
For more info please Contact
07899 784806/07897 362757....
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
Spika Sitta Amtembelea Dr Migiro
Pichani ni Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Mhe.Samuel Sitta(Kushoto) akisalimiana na Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha-Rose Migiro alipomtembelea ofisini kwake,makao makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani.Mheshimiwa Spika yupo Jijini New York kuhudhuria Mkutano wa pili wa kamati ya maandali ya mkutano wa Maspika wa Mabunge Duniani utakaofanyika Julai 2010 huko Geneva.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
Kipanya..
 
Mwandishi: haki Tarehe: Wednesday, November 18, 2009 | kiungo mahususi
MEMORIAL SERVICE
WASHINTON DC..
Tujumuike na familia ya Elias Stafford Mshana(Massawe)
katika ibada jumapili november 22 saa nane mchana(2:00pm) ya kumuombea mama yao mpendwa Bertha Stafford Mshana aliyefariki nov 12/2009 katika hospitali ya KCMC,Moshi Kilimanjaro na kuzikwa november 16/2009,Moshi,Kilimanjaro.

Ibada itafanyikaGood Samaritan Lutheran Church,10110 Greenbelt Road,Lanham,Md,20706.Sisi tulikupenda lakini mwenyezi Mungu amekupenda zaidi,ukae katika amani mpaka hapo mwenyezi Mungu atakapo tukutanisha tena,yeye alitoa na yeye ametwaa,jina lake lihimidiwe.
Kwa maelekezo zaidi,wasiliana:
Marco Mbullu 571 426 7124,
Elvis Saria 301 213 0657,
Elias Stafford 301 646 5683
Ray Abraham 301 793 4467
 
Sunday, November 15, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Seif Amsindikiza Rais Karume Kutunukiwa Shahada

UHUSIANO kati ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Dk Amani Karume na Chama cha Wananchi (CUF), unaonekana kuendelea kuimarika baada ya viongozi wa chama hicho jana kumsindikiza rais huyo katika hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu Maalim Seif jana walimsindikiza Karume katika kutunukiwa shahada hiyo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki.

Baada ya rais huyo wa Zanzibar kutunukiwa shahada hiyo, mshereheshaji alitangaza makundi ya picha za pamoja ambapo kundi la kwanza lilikuwa la Karume na viongozi wa siasa; Kundi hilo ndilo lililowashirikisha pia viongozi wa CUF.

Kabla ya kupiga picha Maalim Seif alikwenda kumpa mkono wa kumpongeza Karume akafuatia Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wakafuatia wengine.

Hata hivyo, viongozi hao wote jana hawakuwa tayari kuzungumzia kwa undani walichozungumza wakati walipokutana.

Rais Karume alisema tofauti kubwa iliyokuwepo visiwani humo ni ya kiitikadi za kisiasa hali ambayo alibainisha kuwa sasa imekuwa historia kutokana na CUF, kutangaza kumtambua rais huyo.

Novemba saba mwaka huu, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif aliwatangazia mamia ya wafuasi wa chama hicho kisiwani Pemba kwamba chama hicho kimeamua kumtambua rasmi Rais Karume.

Pamoja na hatua hiyo ya CUF, kupongezwa na watu mbalimbali zikiwamo taasisi za kimataifa na mabalozi, ilikuwa mwiba kwa wanachama wa CUF, ambao wengi wao waliangua vilio baada ya kusikia kauli ya Seif.

Kauli hiyo mpaka sasa imeibua makundi miongoni mwa wanachama wa CUF, huku baadhi ya wanachama hao wakimuunga mkono Seif na wengine kumpinga.

Akizungumzia hali hiyo jana, Seif alisema kulikuwa na chuki ya dhahiri miongoni mwa Wazanzibari kwa misingi ya kisiasa na kuwa hali hiyo ndiyo iliyofanya watu wakalia kama watoto wadogo, baada ya kusikia kiongozi wao huyo kutangaza kumtambua Rais Karume.

Kwa hatua tuliyofikia tutaiepusha nchi yetu na mambo mengi mabaya, hatua hii imefikiwa kwa maslai ya Zanzibar, tumechoswa na migogoro Zanzibar, nyiye waandhisi simnajua kuwa sisi wazanzibar tuna matatizo yetu wenyewe, basi hayo ndo tunataka tuyamalize, alisema Karume.

Alisema anaamini kuwa yeye na Seif ndio viongozi wakubwa Zanzibar hivyo hatua yao ya kuamua kumaliza tofauti zao za kisiasa itasaidia kuchochea maendeleo ya visiwa hivyo.

Katika hali ambayo haikuzoeleka hapo awali kwa viongozi hao wa CUF wote kwa pamoja walimpongeza Rais Karume kwa kutunukiwa shahada hiyo ya heshima na kusema kuwa alistahili kutokana na juhudi zake za kuvipatia visiwa hivyo amani na maendeleo.

Katika siku za nyuma viongozi hao wa CUF, walionekana kupinga na kukejeli kila kitu kilichokuwa kikifanywa na Serikali ya Mapinduzi na wakati mwingine hata vilivyokuwa vikifanywa na Serikali ya Muungano.

Kwa upande wake Karume alisema kwa sasa wameamua kuachana na siasa ya zamani na kuwa lengo lao ni moja tu la kuipigania Zanzibar na wananchi wake.

Alisema wameamua kushirikiana ili kuhakikisha kuwa chaguzi mbalimbali zinazo fanyika visiwani humo, haziwi chanzo cha mitafaruku bali kuwaunganisha wazanzibari.

Chama cha Wananchi CUF kila wakati kimekuwa kikipinga matokeo yatokanayo na chaguzi mbalimbali hali ambayo wakati mwingine ilisababisha umwagikaji wa damu visiwani humo.

Katika siku za hivi karibuni kulikuwa kunamsuguano mkubwa uliohusu uandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyofanya CFU kutisha umwagikaji mwingine wa damu endapo matakwa yake yasingetekelezwa.

Kutoka Dodoma, Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Mkoani Dodoma jana walifanya maandamano ya kukipongeza Chama Cha Wananachi (CUF) kwa uamuzi wa kumtambua rais wa Zanzibar huku kukiwa na ulinzi mkali wa Polisi.

Maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya bunge mjini Dodoma

yalipokelewa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashid Mohamed katika viwanja wa Mwalimu Nyerere maarufu kama Nyerere Square.

Hata hivyo tofauti na ilivyotarajiwa wakati maanadamano hayo yalipotangazwa na vyombo vya habari, jana wanafunzi waliojitokeza katika maanadamano hayo walikuwa ni wachache sana idadi ambayo haikuzidi wanafunzi 50.

Katika maanadamano hayo wabunge wanne chama cha CUF walifika kwa ajili ya kuwaunga mkono wanafuzni hao ambao walikuwa pamoja na wananchi wachache waliojitokeza.

Wabunge waliokuja mjini hapa jana ni pamoja na Dk Ali Taarabu Ali (Konde),Habibu Juma Mnyaa (Mkanyageni) Salimu Hemedi (Chambani) pamoja na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambae alikuwa mgeni rasmi.

Wabunge hao licha ya kuzungumzia mustakabali mzima wa mazungumzo ya Karume na Seif Shalifu Hamadi, walitumia muda mwingi katika kusifia chama  kwa madai kuwa ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania.

Tangu kuingia kwa mfumo wa siasa za vyama vingi CUF tumekuwa tukiongeza idadi ya wakilishi pamoja na kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguziwa serikali za Mitaa katika ameneo mbalimbali nchini hiyo ni dalili kuwa sisi ndio wapinzani pekee hapa Tanzania,alisema Dk Taarabu.

Kwa upande wake Mnyaa alisema kuwa chama hicho kinachohitaji siasa safi na sio siasa za kuibiana kura kila unapofika uchaguzi.

Mnyaa pia alikosoa mapungufu ya vyama vyote ikiwemo CCM na Cuf kwa kusema kuwa hayana tija kwa wananchi wan chi masikini kama Tanzania.

Kwa ccm alisema kosa lao kubwa ni kitendo cha chama hicho kuamini kuwa kinaweza kila kitu na kwamba hakuna chama kingine kinachoweza kufanya jambo lolote isipokuwa wao hali ambayo alisema inatokana na mawazo finyu.

Aliyataja mapungufu ya cuf kuwa ni pamoja na imani kuwa hakuna kilichofanyika ndani ya ccm wakati yapo mambo mazuri ambayo chama hicho tawala kilishayafanya na hivyo akaomba hayo yaliyofanywa mazuri ni budi yaheshimiwe na kuenziwa.

Akizungumza katika mkutano huo kioongozi wa kabi ya upinzani bungeni aliwataka wanafunzi kutumia elimu yao na maarifa kwa ajili ya kudai mabadiliko ya katiba.

Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa sana na kusema kweli ninyi wasomi ndio mtakaoleta mabadiliko hayo hivi inawaingia akilini kweli uchaguzi kama huu uliofanyika hivi karibuni kusimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu katiba hii inamapungufu makubwa sana,alisema Mohamed.

Alitumia muda huo pia kuwataka wanafunzi pamoja na Watanzania kuendelea kumpigia debe mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahim Lipumba kuwa bado anazo sifa za kugombea urais wa nchi.

Kiongozi huyo alisema kuwa Lipumba ameshaanza kufahamika na wananchi hivi sasa na hivyo wawapuuze wale wanaosema kuwa asigombee urais kwa kisingizio cha kuwa ameishiwa sera jambo alilosema kuwa hata Viongozi wengi barani Afrika huingia kwa kutambulika kwanza.

Imeaandikwa na Fredy Azzah, Habel Chidawali na Neema Mathias

 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi

Dk Slaa Atajwa Kugombea Urais Mwakani

VUGUVUGU la kupata mgombea wa urais mwakani ndani ya Chedema linadaiwa kuanza huku Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa akipendekezwa kuchukua nafasi hiyo.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zimeeleza kuwa Dk Slaa ametajwa kuwania nafasi hiyo akipambana na kiongozi mmoja wa juu serikalini ambaye ni mwanachama wa Chadema.

Mchakato wa kutafuta mgombea huyo, umeanza kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro hivyo kukosa sifa kikatiba kugombea urais.

Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye hakutaka kutajwa gazetini, zinaeleza kuwa suala hilo limekuwa likijadiliwa katika vikao vya juu vya chama bila mwafaka.

Ni kweli kuna viongozi wanamtaka Dk Slaa agombee pia kuna kigogo mmoja ameonyesha nia ya kuja Chadema na kugombea na kuna wanasiasa wengine maarufu hawajatoa uamuzi, lakini mapema mwakani nadhani tutakuwa katika hali nzuri ya kujua nani atagombea,alisema kiongozi huyo.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Chadema imekuwa na wakati mgumu kumtangaza Dk Slaa kuwa atagombea urais mwakani hasa kutokana na hofu ya kupoteza Jimbo la Karatu.

Pia hofu nyingine inatokana na baadhi ya wana CCM kuanza kuonyesha nia ya kuondoka katika chama hicho kujiunga na Chadema, kutokana na mgogoro unaoendelea kukitafuna chama chao.

Inaelezwa kuwa kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo ndani ya chama hicho, huenda makada maarufu wakaamua kujitoa na kujiunga na upinzani, hali ambayo inaweza kuwafanya wakapata mgombea urais.

Akihutubia wananchi wa Karatu wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Phillemone Ndesamburo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua mtu ambaye ataletwa badala ya Dk Slaa kwa sababu chama kimeamua kumpa majukumu mengine.

Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Titus Lazaro ambaye amekuwa akitajwa

kutaka kumrithi Dk Slaa.

Alisema hadi sasa anaamini hakuna mtu wa kumrithi Dk Slaa Karatu hivyo ni

bora akaachwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Lazaro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuanza kutafuta mrithi wa Dk Slaa sasa kunaweza kulipoteza jimbo hilo ambalo limekuwa likinyemelewa na CCM.

Mimi sijafikiria kugombea ubunge kama Dk Slaa akigombea urais kwani najua ugumu wa jimbo hili na mikakati mingi ya CCM kulitaka jimbo la Karatu alisema Lazaro.

Hata hivyo,kwa upande wake Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa bado hajaamua kugombea urais mwakani.

Mimi huwa sipendi kuzungumza bila ya kufanya utafiti..ni kweli watu wanasema nigombee ila bado sijaamua na jambo hili linahitaji utafiti kwanza,alisema Dk Slaa.

Dk Slaa ambaye katika siku za hivi karibuni, amekuwa mmoja wa viongozi wanaoheshimika na wenye msimamo mkali ndani ya chama hicho na bungeni, alisema muda wa kutangaza kugombea urais haujafika na suala la urais ni zito sio la kusema bila kuwa na mikakati.

Umaarufu wa Chadema katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukiongezeka hasa kutokana na kuanzisha Operesheni Sangara nchi nzima ambayo imekifanya chama hicho kupata wafuasi wengi.

Chadema ilianza kuweka mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ikimsimamisha kuwania kiti hicho, Freeman Mbowe ambaye pia alisimama mwaka 2005, huku ikiweka rekodi ya chama cha upinzani kutumia helikopta katika mikutano yake ya kampeni.

Mkakati wa kumsimamisha Dk Slaa ni kutaka kuongeza idadi ya wabunge baada ya kumtumia Mbowe mara mbili.

 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Dk. Salim Ahmed Salim Akimpongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Abeid Aman Karume Baada Ya shahada ya Heshima.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dk. Salim Ahmed Salim akimtunuku shahada ya Heshima Rais wa Zanzibar, Dk. Abeid Aman Karume wakati wa mahafali ya 7 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam, jana. Chini Dk. Salim Ahmed Salim akimpongeza Mh. Karume kwa kutunukiwa shahada hiyo.
Rais Amani Karume Atunukiwa Shahada Ya Heshima
 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Elizabeth akiwa na mbunifu wa mitindo Ally Rhemtullah
Aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Africa, Elizabeth Gupta akionyesha umahili wake wa kucheza muziki akiwa na Joketi katika ukumbi wa Club Bilicanas, Ijumaa usiku wakati wa hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Multchoice Tanzania.
Elizabeth akijimwayamwaya na wadau
Miss TZ 2008 Nasreem Karim akiwa na Miss TZ namba 2 wa mwaka 1994 Lucy Kihwele na Joketi wakimwangalia Elizabeth akijiachia kwenye mnuso wake
Mnuso Wa Kumkaribisha Nyumbani Elizabeth
 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Rais Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Philipo Pagali mkazi wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo ambaye nyumba yake aliyokuwa anaishi iliharibiwa vibaya na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.Jumla ya nyumba 51 ziliezuliwa mapaa na kuharibiwa mapaa na kusababisha watu zaidi ya 190 kukosa mahali pa kukaa na kulazimika kuhifadhiwa na majirani
Rais Jakaya Kikwete akukagua baadhi ya nyumba zilizoharibiwa vibaya na mvua kubwa iliyombatana na upepo mkali katika kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo hivi karibuni wakati alipotembelea kijiji hicho leo asubuhi.Jumla ya nyumba51 ziliharibiwa vibaya na mvua hiyo na kusababisha watu zaidi ya 190 kukosa makazi na kuhifadhiwa na majirani. Picha na Freddy Maro.
Rais Jakaya Kikwete Atembelea Msoga Kujionea Madhara Ya Mvua Kubwa.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Reli Bado Ipo Jamani Haijafa Bado.
Mfanyakazi wa kampuni ya reli Tanzania (TRL) akiendelea na kazi ya ufundi katika karakana ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku moja baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kutangaza kutomtambua muwekezaji wake. Picha na peres mwangoka
 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Natumai Hii Shule Itakuwa Inaitwa "Mbuyuni Primary School"

Mvua ikinyesha: Mwisho wa masomo

Mwalimu , Albert Juakali wa shule ya msingi Iboma iliyopo kijiji cha Udinde Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya Mti wa Mbuyu kama alivyokutwa na Mpigapicha wetu. Picha na Brandy Nelson

 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Makufuli Ya Majembe Yaondolewa Dowans.
Lango kuu la kuingilia katika eneo la mitambo ya Kampuni Dowans jana likiwa limeondolewa makufuli yaliyokuwa yamewekwa juzi na wakala wa kukusanya madeni sugu, Kampuni ya Udalali wa mahakama ya Majembe Auction Mart juzi. Picha na Silvan Kiwale
 
Mwandishi: haki Tarehe: Sunday, November 15, 2009 | kiungo mahususi
Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania.
Mtoto wa mtaani akiwa amechapa usingizi katika nguzo ya taa ya barabarani iliyoanguka katika barabara ya Bibi Titi Mohammed jijini Dar es Salaam bila kujali usalama wake kutokana magari kupita karibu yake. Picha na Fidelis Felix
 
Friday, November 13, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
Naomi Campbell Afanya
Vitu Vyake Bongo..
Naomi Campbell akifanya vitu vyake jukwaani wakati wa onyesho maalum lililoandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya The White Ribbon Alliance for Safe Motherhood(WRA)nchini lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Hoteli ya Movenpick
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiongea na Mwanamitindo wa kimataifa Naomi Campbell wakati wa onyesho la mavazi la The White Ribbon Alliance for safe Motherhood lililofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick usiku wa kuamkia leo taasisi hiyo inajishughulisha na kampeni ya uzazi salama kwa wakima mama wajawazito katikati ni mwanamitindo wa Face Of Afrika kutoka Zimbabwe Tollar Kelle, kushoto ni Franco Tramontana na kushoto ni Mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali.
Mtangazaji wa East Africa Televition Deogratius Kithama akifanya mahojiano na mwanamitindo Naomi Campbell usiku wa kuamia leo.Picha zote kwa Msaada wa Mdau John Bukuku
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
Mmoja kati ya wafanyakazi wa Bahari Foods jijini
Dar es Salaam akipanga vizuri samaki hao kwenye moja ya Mafriji
Kiwandani Hapo
----
Ugawaji Wa Samaki Wakwama
Jana

Na Festo Polea na Tumsifu Sanga
UGAWAJI wa tani 296.32 za samaki waliovuliwa kwa njia haramu katika ukanda wa Tanzania kwenye Bahari ya Hindi uliopangwa kufanyika jana,umekwama.Samaki hao maarufu kama 'Samaki wa Magufuli',hawakugawiwa jana kwa taasisi zilizoteuliwa kupata mgawo kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.
Majira ya saa 4:00 asubuhi waandishi wa habari na baadhi ya wananchi walifika katika kiwanda cha Bahari Foods wakisubiri zoezi la ugawaji wa samaki hao lianze,lakini muda ulipita bila matumaini ya kuwaona samaki hao zaidi ya taarifa kutoka kwa walinzi wa kiwanda hicho kueleza kuwa zoezi hilo limesitishwa hadi litakapopangiwa siku nyingine.Kwa habari zaidi bofya na Endelea.>>>>>>>>
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya IPTL inayozalisha Umeme Nchini baada ya kutembelea Mitambo hiyo jana Tegeta Jijini Dar es Salaam.Picha na Enance Ng'ingo
Waziri Ngeleja Atembelea
Mitambo ya IPTL jijini..
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
Rais jakaya kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa nchi ya Rwanda Mheshimiwa Fatuma Ndangiza Nyirakobwa na baadaye Rais kikwete alifanya mazungumzo na Balozi huyo,ikulu Jijini Dar es Salaam Jana
Rais Kitwete Apokea Hati
za Utambulisho..
Rais Jakaya Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Marekani hapa Nchini Mheshimiwa Alfonso Lenhardt ikulu jana jijini Dar es Salaam.Baadaye Rais kikwete alifanya mazungumzo na Balozi huyo.Picha na Freddy Maro/Ikulu
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
Maafa Wilayani Same
Matowo kutokea Same.
SIMANZI na vilio jana vilitawala kwenye mazishi ya watu 2O waliofariki dunia kwa kufunikwa na kifusi kilichoporomoka mlimani na kufukia nyumba zao usiku wa manane katika Kata ya Mamba Miamba,wilayani Same,Kilimajaro.Gazeti la Mwananchi lilishuhudia watu zaidi ya 1,000 waliokusanyika katika msiba huo mkubwa wakiwa wamefunikwa na simazi,huku wakilia kwa uchungu kutokana na kupoteza ndugu zao katika mkasa huo wa kutisha.Asilimia kubwa ya watu walionyesha masikitiko yao,hasa kwa familia ambayo imepoteza watu 15 na kati ya hao wanne hawajapatikana mpaka sasa.

Wanachi hao waliiomba serikali iwasaidie kutafuta miili ya watu hao na ikiwezekana watumie kikosi cha mbwa ili kubaini mahali ilipo.Elineema Shambi,mmoja wa ndugu wa wanafamilia 15 waliofariki dunia na ambaye alinusurika kwa vile alikuwa amekwenda mjini Moshi kwa shughuli za kibiashara,alisema kwa majonzi kwamba amepoteza mke na watoto wake wanne ambao walifukiwa na kifusi hicho.

Alisema alikwenda mjini Moshi kununua bidhaa za kuuza,na kesho yake asubuhi alipigiwa simu na kuondoka mara moja. Alieleza kuwa alipofika alikuta nyumba yake imefunikwa kabisa kiasi cha kutoonyesha kama kulikuwa na nyumba na mwili wa mkewe ulikuwa haujapatikana hivyo akasaidia kuutafuta na kuupata pamoja na miili ya watoto wake.Alifahamisha kuwa yeye ni mmoja kati ya ndugu wa watu 15 waliofariki katika tukio hilo la kutisha.

Akisimulia juu ya maporomoko hayo,alisema,dalili za mlima huo kuporomoka zilianza kuoneka mwaka jana kwa kuwa kulikuwa na ufa,hata hivyo hakueleza kwamba ni kwa nini hawakuhama katika eneo.Akiunga mkono maelezo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Monica Mbega alibainisha kuwa wananchi wa Kata ya Mamba Miamba walishaona dalili za kuporomoka kwa mlima ulioua watu 20,tangu mwaka jana,lakini hawakuchukua tahadhari.
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
Nipe Pesa Zangu..
Mfanyakazi wa Kampuni ya kuegesha magari nchini TPS) akimkunja kijana anayeshughulika na kuegesha magari katika mtaa wa Samora,walikuwa wakigombania fedha ambazo inasemekana kuwa kijana huyo alichukua kutoka kwa mteja aliyeegesha gari lake mahala hapo.Picha na Evance Ng’ingo
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
5th DEC 2009 TANZANIA INDEPENDENCE CELEBRATION IN LONDON
BONGODJS PROUDLY PRESENTS CELEBRATION OF TANZANIA INDEPENDENCE DAY ON SAT 5TH DECEMBER 2009 @ THE PRESTIGEOUS LA ROYALE BANQUENTING SUITES 819-821 HIGH ROAD TOTTENHAM LONDON N17 8ER FROM 7PM-3AM FOR ONLY£15 COME AND ENJOY LIVE BAND BONGODJS ON THE MIX,PS PASS THE MESSAGE AROUND!SPECIAL NITE NOT TO BE MISSED!!! SPONSORED BY SWIFT FREIGHTS UK,TZUK.com &BONGOTIMES
 
Mwandishi: haki Tarehe: Friday, November 13, 2009 | kiungo mahususi
United Against Malaria..
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk.Asha-Rose Migiro akipiga danadana mbele ya mtoto Charles Ssali (12)toka Uganda ambaye ni Balozi maalum wa Muungano dhidi ya Malaria (United Against Malaria)mtoto huyo alipomtembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa,jijini New York,leo.Wengine ni Bw.Robert Skinner kutoka taasisi ya Umoja wa Mataifa na Bw.Herve Verhyoosel kutoka Ushirikiano wa Kutokomeza Malaria(Roll Back Malaria Partnership).
 
Thursday, November 12, 2009
Mwandishi: haki Tarehe: Thursday, November 12, 2009 | kiungo mahususi
President Jakaya Kikwete visited
Agricultural Products Company
in Misri
President Jakaya Kikwete(left)listens to the Chairman of Maghraby Agricultural Products Company,Mr Sherif Maghraby,showing items produced and processed by the firm for export. President Kikwete,who is in Egypt on official visit,visited the company located in Nobaria, northen Cairo yesterday.Photo by Freddy Maro/State House